Tuesday, January 14, 2020

Job Opportunity at Grumeti Fund Trust, Deadline 18 January 2020

GRUMETI FUND TRUST.

Grumeti Fund Trust inatangaza nafasi za kazi zifuatazo;

Askari wa wanyamapori
Majukumu ya Askari wa wanyapori:

Majukumu ya msingi kwa Askari wa wanyapori ni kufanya kazi – kwa kushirikiana na wadau wa Serikali wa

 • Grumeti Fund kuhakikisha usalama kwenye eneo la hifadhi la Grumeti-Ikorongo. Askari wa wanyapori wana
 • wajibu wa kuhahakikisha kuwepo kwa maadili kwenye eneo la hifadhi la Serengeti, hii inajumuisha
 • kuhakikisha kunakuwepo na mazingira ya usalama wa wanyamapori na kwa uoto wa asili.
 • Askari wa wanyapori wana wajibu wa kuzuia vitendo vyovyote vilivyo kinyume na sheria na vilevile kuzuia vitendo vyovyote vya ujangili ndani ya eneo la hifadhi. Watakuwa chini ya utawala na watawajibika kutoa taarifa ya
  vitendo vyovyote vilivyo kinyume na sheria kwa utawala wa Grumeti Fund na kwa wadau wa Serikali. Tarehe ya tangazo 05 /01/2020
  Nafasi za kazi Askari wa wanyamapori Idara husika Kuzuia Ujangili Kituo cha kazi Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa Mara, Tanzania Msimamizi wa kazi Mkuu wa Idara ya Kuzuia Ujangili (Anti-Poaching Manager)

Ufafanuzi wa majukumu:
 Kushiriki kwenye mafunzo ya majuma sita (6) ya uteuzi
 Kufanya doria kwenye eneo la hifadhi kwa jitihada za kuhakikisha kuwa liko salama kwa wanyamapori
 Kuzuia vitendo vyovyote Vilivyo kinyume na sheria kwenye eneo husika la hifadhi kwa mfano ujangili,
uchungaji mifugo usioruhusiwa, ukataji wa miti na utengenezaji wa mkaa na kutembea maeneo ya hifadhi,
 Kusaidia kuwakamata majangili kwenye eneo la hifadhi
 Kutoa taarifa zozote za ujangili au za matendo yoyote yaliyo kinyume na sheria ambayo yatajulikana
 Kusaidia usalama wa maisha ya watu, mazao na mifugo iliyoko karibu na eneo la hifadhi inayoweza kuvamiwa na wanyamapori
 Kuwa tayari kufanya kazi muda wowote mchana au usiku
 Kufanya kazi zozote za idara kama zitakavyoelekezwa na utawala

Sifa za waombaji

 1. Angalau aliyehitimu na mwenye cheti cha elimu ya kidato cha nne
 2. Angalau mhitimu wa ngazi ya Stashahada kwenye usimamizi wa wanyamapori (Wildlife Management)
 3. Aliyehitimu mafunzo kamili ya jeshi la kujenga Taifa (JKT) ya kuanzia miezi sita (6). Wenye Mafunzo ya miezi mitatu hawataruhusiwa.
 4. Mwenye uwezo wa kuwasiliana vizuri kwa Kiingereza na Kiswahili kwenye kuandika na kuzungumza
 5. Mwenye uwezo wa kuandaa taarifa ya kazi vizuri na inayoeleweka vema.
 6. Muombaji awe na umri wa miaka 23 mpaka 35
 7. Muombaji ni lazima awe na moyo wa kuwapenda wanyamapori Vigezo vya uteuzi
 8. Waombaji wa nafasi hizi za kazi ni lazima wawe wakakamavu, wenye afya njema ya mwili na ya akili
 9. Waombaji wote wa nafasi hizi ni lazima wawe tayari kupimwa afya, upimwaji huu utafanywa na wataalamu wa afya wa kampuni
 10. Waombaji wote wa nafasi hizi na ambao wataitwa kwa ajili ya usaili ni lazima wawe tayari kushiriki kwenye mafunzo ya muda wa majuma sita (6) ya ukakamavu na kuchunguzwa tabia zao. Mafunzo haya ya muda mfupi ni ya mchujo na hayatoi kibali cha kuajiriwa.
 11. Waombaji wote watakaoitwa kwenye usaili watapaswa kujigharamia gharama za usafiri. Malazi na chakula vitatolewa kituoni bila gharama yoyote. Jinsi ya kutuma maombi yako: Ikiwa unapenda kuomba nafasi hizi za kazi na umekidhi vigezo kama vilivyoainishwa hapo juu basi fuata masharti
  yafuatayo;
 12. Andika barua ya maombi ya kazi na uambatishe taarifa zako binafsi zinazoeleweka vyema (CV), cheti cha kuzaliwa, pamoja na vyeti vya kuhitimu taaluma yako. Taarifa zako binafsi (CV) ni lazima zioneshe mahali unakoishi kwa sasa, namba zako za simu zinazopatikana pamoja na anuani na namba za simu za watu angalau watatu (3) wanaokufahamu vizuri na wanaoaminika ambao watakudhamini.
 13. Waombaji wote waliohitimu mafunzo ya kujenga taifa (JKT) ni lazima waambatishe barua ya utambulisho kutoka JKT pamoja na cheti cha kuhitimu mafunzo hayo.
 14. Vyeti vyote vitakavyowasilishwa vitafanyiwa uchunguzi wa hali ya juu, muombaji atakayewasilisha cheti cha uongo au atakayetoa taarifa za uongo ataondolewa mara moja na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
 15. Maombi yote yatumwe kwa Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu; ama kwa anuani ya barua elekroniki (email) ambayo ni: jobapplications@grumeti.singita.com au kwa njia ya Posta kwenda kwa:

Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu
Grumeti Reserves Ltd
S.L.P. 65
Mugumu, Mara, Tanzania.

MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI TAREHE 18/01/2020, SAA 11.00 JIONI.

Grumeti Fund Trust haina ubaguzi wa aina yoyote kwenye kutoa ajira.


To advertise your business Download Maelewano APP or visit Maelewano Website

The post Job Opportunity at Grumeti Fund Trust, Deadline 18 January 2020 appeared first on Ajira Zetu.

The post Job Opportunity at Grumeti Fund Trust, Deadline 18 January 2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.source http://ajira-nafasizakazitz.com/8531/