Friday, April 3, 2020

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Marine Service Company Limited (MSCL)

JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.Na.EA.7/96/01/K/179 02 APRILI, 2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MARINE SERVICES COMPANY LIMITED (MSCL) anapenda kuwataarifu waombaji kazi
waliotuma maombi ya kujaza nafasi wazi za Shirika hilo, kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 07 hadi 09 Aprili, 2020 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi Waombaji Kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili utafanyika kuanzia tarehe 07 hadi 09 Aprili, 2020 kama ilivyoainishwa kwenye tangazo hili.
ii. Muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila kada;
iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au
Hati ya kusafiria;
v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada nakuendelea kutegemeana na sifa za kazi husika iliyoanishwa kwenye tangazo;
vi. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form IV and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;

vii. Kila Msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
viii. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
ix. Kwa Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU,NACTE na NECTA);
na
x. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya Tangazo husika.
xi. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma
wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Marine Service Company Limited (MSCL) appeared first on Ajira Zetu.

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Marine Service Company Limited (MSCL) appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.source http://ajira-nafasizakazitz.com/15044/