Saturday, May 30, 2020

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI Tarehe 06 – 17 Juni, 2020

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.NaEA.7/96/01/K/208 29 Mei, 2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Taasisi mbalimbali zilizoorodheshwa kwenye ratiba ya uasili, anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 06 hadi 17 Juni, 2020 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i. Usaili utafanyika kuanzia tarehe 6 hadi 17 Juni, 2020 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;

ii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask) na kuzingatia masharti mengine ya kujikinga na COVID 19 KAMA YALIVYOAINISHWA NA WIZARA YA AFYA awapo eneo la usaili,
iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na ama Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha kazi cha taasisi inayojulikana, Kitambulisho cha Uraia ,Hati ya kusafiria au Leseni ya Udereva
v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
vi. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
vii. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
viii. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
ix. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (NECTA NACTE na TCU);
x. Waombaji kazi ambao majina yao hayaonekani katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
xi. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

RATIBA YA USAILI

KUSOMA RATIBA NA MAJINA PAKUA PDF HAPO CHINI

The post Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI Tarehe 06 – 17 Juni, 2020 appeared first on Ajira Zetu.

The post Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI Tarehe 06 – 17 Juni, 2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.source http://ajira-nafasizakazitz.com/17476/