Wednesday, May 27, 2020

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Tarehe 1 – 2 Juni 2020, Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa

HALMASHAURI YA WILAYA YA KONGWA

HW/KOG/S.20/33/159 25 MEI, 2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi ya Utendaji wa Kijiji Daraja la III kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 01 hadi 02 Juni, 2020. Wasaili wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
(i) Usaili wa Mchujo utafanyika tarehe 01 Juni, 2020 kuanzia saa 1.30 Asubuhi katika Shule ya Sekondari ST.FRANCIS-KONGWA na Usaili wa Mahojiano
utafanyika tarehe 02 Juni, 2020 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.
(ii) Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask) na kuzingatia maelekezo yote ya kujikinga na Corona.
(iii) Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
(iv) Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na ;Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha Kazi, Kitambulisho cha Uraia au
Hati ya Kusafiria;
(v) Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV au VI, Astashahada na “Transcript”.
(vi) Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV au VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
(vii) Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
(viii) Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU , NACTE na NECTA);
na;
(ix)Waombaji kazi ambao majina yao haya kuonekana katika tangazo hili watambue kuwa
hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
(x) Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
(xi)Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika ambaye ni NECTA.
(xii)Orodha ya waombaji walioitwa kwenye usaili inapatikana kwenye tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ambayo ni www.kongwadc.go.tz pamoja na
mbao za matangazo za Halmashauri.
(xiii) Tahadhari usaili utafanyika kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa Umma, kuna matapeli wanaotumia majina ya watu na vyeo vya
watu kwa lengo la kujipatia fedha kuweni makini na matapeli hao.

KUSOMA MAJINA HAYO BOFYA PDF HAPO CHINI

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Tarehe 1 – 2 Juni 2020, Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa appeared first on Ajira Zetu.

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Tarehe 1 – 2 Juni 2020, Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.source http://ajira-nafasizakazitz.com/17347/