Saturday, June 13, 2020

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili TANESCO Tarehe 20 hadi 23 Juni, 2020

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.NaEA.7/96/01/K/215

12 Juni, 2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibuwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishiwa Umma kwa niaba ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 20 hadi 23 Juni,2020 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usailihuo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i.Usaili utafanyika kuanzia tarehe 20 hadi 23 Juni, 2020 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwakila Kada;
ii.Kila Msailiwa anapaswa kunukuu kwa usahihi namba yake ya usaili wa mchujo na kwa Madereva wenye usaili wa Vitendo pia, namba hizo zinapatikana kwenye akaunti ya kila Msailiwa katika mfumo wa maombi ya kazi.
iii.Kila msailiwa ana takiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa(Mask);
iv.Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
v.Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:-Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hatiyakusafiria;
vi.Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
vii.Wasailiwa watakao wasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
viii.Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi; ix.Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili; x.Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika(kama TCU, NACTE auNECTA);
xi.Waombajikazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapo tangazwa nakuzingatia mahitaji ya tangazo husika. xii.Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi

KUSOMA MAJINA NA RATIBA PAKUA PDF HAPO CHINI

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili TANESCO Tarehe 20 hadi 23 Juni, 2020 appeared first on Ajira Zetu.

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili TANESCO Tarehe 20 hadi 23 Juni, 2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.source http://ajira-nafasizakazitz.com/18178/