Saturday, June 13, 2020

Tangazo la Kuitwa Kwnye Usaili Utumishi ( MNH, STAMICO, TARI,TIRA, TPRI,TCAA MDAs & LGAs) Tarehe 18hadi 26 Juni, 2020

JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA

OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.NaEA.7/96/01/K/217

12 Juni,2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Muhimbili National Hospital (MNH), State Mining Corporation (STAMICO), Tanzania Agricultural Research Institute (TARI), Tanzania Insurance Regulatory Authority (TIRA), Tropical Pesticides Research Institute (TPRI), Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na MDAs & LGAs anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 18hadi 26 Juni, 2020 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi Waombaji Kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i.Usaili utafanyika kuanzia tarehe 18hadi 26 Juni, 2020 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kilaKada;
ii.Kila Msailiwa anapaswa kunukuu kwa usahihi namba yake ya usaili wa Mchujo na na kwa wale wenye Vitendo pia watafanya hivyo wakipita hatua ya awali, namba hizo zinapatikana kwenye akaunti ya kila Msailiwa katika mfumo wa maombi ya kazi wa Sekretarieti yaAjira.
iii.Kila Msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa(Mask);
iv.KilaMsailiwaanapaswakuwanakitambulishokwaajiliyautambuzi;
v.Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:-Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati yakusafiria;
vi.Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
vii.Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NAUSAILI;
viii.KilamsailiwaatajigharamiakwaChakula,UsafirinaMalazi;
ix.KilaMsailiwaazingatietarehenamahalialipopangiwakufanyiausaili;
x.Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwanakuidhinishwanaMamlakahusika(TCU,NACTEauNECTA);
xi.Waombaji kazi ambao majina yao haya kuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazohusika.
xii.Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyiakazi.

KUSOMA MAJINA HAYO PAKUA PDF HAPO CHINI

The post Tangazo la Kuitwa Kwnye Usaili Utumishi ( MNH, STAMICO, TARI,TIRA, TPRI,TCAA MDAs & LGAs) Tarehe 18hadi 26 Juni, 2020 appeared first on Ajira Zetu.

The post Tangazo la Kuitwa Kwnye Usaili Utumishi ( MNH, STAMICO, TARI,TIRA, TPRI,TCAA MDAs & LGAs) Tarehe 18hadi 26 Juni, 2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.source http://ajira-nafasizakazitz.com/18175/