Friday, July 31, 2020

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Utumishi Kuanzia Tarehe 6 – 21 Agosti 2020

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.NaEA.7/96/01/K/25530

Julai, 2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya“Land Transport Regulator Authority”(LATRA), “Tanzania Shipping Agencies Corporation”(TASAC), Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi(NAOT), Chuo Kikuu cha Mzumbe(MU), Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA), “Livestock Training Agency”(LITA), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), “Tanzania Meteorology Authority”(TMA), Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE), Shirika la Mzinga, Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI)na “Institute of Accountancy Arusha”anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili wavitendo unatarajiwa kufanyi katarehe 6-21 Agosti, 2020, usaili wa kuandika unatarajiwa kufanyika tarehe08-14Agosti, 2020nakufuatiwa na usailiwa mahojiano ambao utafanyika tarehe10-11 Agosti, 2020.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i.Usaili wa vitendo utafanyika tarehe 6-21 Agosti, 2020kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili, muda na sehemuambapo usaili huo utafanyika umeainishwa kwa Kada zinazohusika;
ii.Usaili wa mchujo (kuandika)utafanyika tarehe 08Agosti, 2020 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;
iii.Kila msailiwa ahakikishe anaingia kwenye akaunti yakena kunakilinamba ya kufanyia mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili;
iv.Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa na kuzingatia masharti mengine ya kujikinga na COVID 19 kama yalivyoainishwa na Wizara ya Afya awapo eneo la usaili,
v.Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
vi.Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja naamaKitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha kazicha taasisi inayojulikana, Kitambulishocha Uraia ,Hati ya kusafiria au Leseni ya Udereva;
vii.Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
viii.Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
ix.Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;x.Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;xi.Kwa waombajiwaliosomanje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (NECTA,NACTE auTCU);
xii.Waombaji kazi ambao majina yao hayaonekanikatika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
xiii.Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

KUSOMA MAJINA HAYO PAKUA PDF HAPO CHINI

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Utumishi Kuanzia Tarehe 6 – 21 Agosti 2020 appeared first on Ajira Zetu.

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Utumishi Kuanzia Tarehe 6 – 21 Agosti 2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.source http://ajira-nafasizakazitz.com/20322/