Thursday, August 27, 2020

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Utumishi Tarehe 04 Septemba,2020

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAISSEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.NaEA.7/96/01/K/26926Agosti,2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishiwa Umma kwaniaba ya BUNGELA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MAMLAKA YA MAJI SAFI NA TAKA DODOMA (DUWASA), CHUOCHA ELIMU YA BIASHARA (CBE) PAMOJA NA TAASISIYA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM (DIT), anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa tarehe 04 Septemba,2020 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i.Usaili utafanyika 4Septemba , 2020kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwakilaKada;

ii.Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask);
iii.Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwaajiliya utambuzi; Vitambulisho vinavyokubalika ni pamojana:
-Kitambulisho cha Mkazi,
-Kitambulisho cha Mpigakura,
-Kitambulisho cha kazi,
-Kitambulisho cha Uraia au

 • Hatiyakusafiria;
  iv.Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
  v.Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo zakidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
  vi.Kilamsailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
  vii.KilaMsailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyiausaili;
  viii.Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikisheVyetiv yaovimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlakahusika(kama TCU, NACTE auNECTA);
  ix.Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hiliwatambue kuwa hawakukidhivigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazohusika.
  x.Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi

KUSOMA MAJINA HAPO PAKUA PDF HAPO CHINI

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Utumishi Tarehe 04 Septemba,2020 appeared first on Business Solutions.

The post Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Utumishi Tarehe 04 Septemba,2020 appeared first on Ajira - Nafasi za kazi Tanzania 2019.source http://ajira-nafasizakazitz.com/22013/